Wilaya ya Mtwara Vijijini

Mahali pa Mtwara Vijijini (kijani) katika mkoa wa Mtwara.

Wilaya ya Mtwara Vijijini ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Mtwara.

Wilaya hii imepakana na Msumbiji upande wa kusini, Wilaya ya Tandahimba upande wa magharibi, Mkoa wa Lindi upande wa kaskazini na Mtwara Mjini pamoja na Bahari Hindi upande wa Mashariki.

Eneo la wilaya ni kilomita za mraba 3,597 km². Mto mkubwa ni Ruvuma ambao ni pia mpaka wa Msumbiji.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 158,504 [1]. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 228,003 [2] waishio humo.

Wakazi walio wengi ni Wamakonde na Wamakua.

  1. https://www.nbs.go.tz/
  2. "Sensa ya 2012, Mtwara DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-17.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy